Kauli ya Mkwasa na kocha wa Nigeria kufuatia mchezo wa jana, zote zipo hapa
Baada ya mchezo kumalizika kati ya Stars dhidi ya Nigeria, kocha mkuu wa
Taifa Stars Charles Boniface Mkwasa amesema hawakuingia kichwakichwa kwenye mechi hiyo bali walikuwa na mipango lakini amerishwa na matokeo hayo kwani bado anajenga timu na kwa sasa anajipanga kwa ajili mechi zijazo.
“Nashukuru Mungu kwa matokeo mazuri tuliyopata japo sio mazuri sana lakini kwangu mimi ni mazuri kwasababu ndio kwanza tunajenga timu kama mlivyoona wengine ndio kwanza wanacheza mechi kubwa kama hii lakini wamejitahidi vya kutosha sana”, amesema Mkwasa.
“Hii mechi tumecheza kwa tahadhari sana kwasababu hatukuwa tumewaona Nigeria wakicheza. Mechi hii tulikuwa tunacheza nyumbani na timu imekuwa haifanyi vizuri kwa mechi kadhaa zilizopita kwa hiyo tulikuwa tunacheza kwa nidhamu ya ulinzi kuliko kucheza open game, kwahiyo kipindi cha pili tukacheza open game”.
“Hatuikuingia kichwakichwa, tuliingia na mipango ambayo tulikuwa tumeiweka pengine tungefunguka mapema tungeweza kufungwa goli la mapema kwahiyo mwanzoni tulicheza kwa tahadhari kuweza kumiliki katikati ili badae tucheze open football”.
Kwa upande mwingine kocha wa Nigeria nae alitoa tathmini yake juu ya mchezo huo
Kocha wa Nigeria Sunday Oliseh amekiri kuwa timu yake haikucheza vizuri kwenye kipindi cha kwanza na ilitokana na kubanwa na Stars na aliipongeza Stars kwa kiwango walichokionesha kwa kutoa upinzani wa nguvu kwa ‘Super Eales’ . Olise na yeye kwa upande wake amesema bado anajenga timu yake na kwamba wachezaji wake walifanya mazoezi ya pamoja kwa siku mbili tu kabla ya mchezo dhidi ya Stars.
“Kipindi cha kwanza hatukucheza vizuri lakini tuliporudi kipindi cha pili tulibadilika na kucheza vizuri, nawapongeza wachezaji wangu kwasababu hii ni timu mpya lakini nawapongeza pia Tanzania wametupa upinzani wa nguvu”.
“Wachezaji wangu wamefanya vizuri utaona kwa upande wetu ujenzi wa timu unaendelea na nimefurahishwa na mchezo wa leo umetupa pointi moja leo na tunajipanga kwa ajili ya mchezo wetu dhidi ya Tanzania watakapokuja Nigeria”.
“Niliogopa kipindi cha kwanza kwasababu hatukucheza kwa kiwango chetu kwasababu tulibanwa, lakini kipindi cha pili tulirejea kwenye kiwango chetu. Timu haikuwa pamoja kwa muda mrefu, wamefanya mazoezi kwa siku mbili tu. Kuondoka hapa na pointi moja nadhani ni kitu kizuri kwa
timu”.
Ungana nasi kupitia Facebook kwa ku like ukurasa wetu wa Kandanda 24 na Twitter @Kandanda 24
Kauli ya Mkwasa na kocha wa Nigeria kufuatia mchezo wa jana, zote zipo hapa
Reviewed by Steve
on
Sunday, September 06, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Sunday, September 06, 2015
Rating:




No comments:
Post a Comment