Propellerads

Rooney: Sina tatizo na Sir Alex Ferguson



Mshambuliaji wa Man United, Wayne Rooney amesisitiza kua hana
tatizo lolote na aliyekua kocha wa klabu hiyo Sir Alex Ferguson kufuatia kutoelewana kwa wawili hao mwaka 2013.

Rooney ambaye alihamia Man United akitokea Everton mwaka 2004 alikosolewa na Ferguson alipoomba kuhama klabu hiyo wakati wa msimu wa mwisho wa kocha huyo ambapo sasa kapteni huyo wa England amedai hakua na tatizo nae na amemwita  greatest "of all time".

Akiongea katika mkutano na waandishi wa habari kabla ya mechi na Swutzerland, Rooney alisema "Sidhani kama kuna mtu anajua mambo yaliishaje. Tulikua na tofauti kimtazamo. Hii ni kawaida. Muulize Roy (Hodgson) ana tofautiana na wachezaji wengine. Hiyo ni sehemu ya mpira.

"Mimi sio mtu pekee niliekua ana tofauti na Sir Alex Ferguson, lakini bado naweza kusema alikua ni kocha bora wa wakati wote ( greatest manager of all time)

"Bado namuona Sir Alex akiwa kwenye baadhi ya michezo pia hua anasafiri na sisi michezo ya Ulaya. Sio kwamba hatupendani ila tulikua na tofauti. Hiyo ni kawaida."

Rooney aliteuliwa kua kapteni wa Man United mwaka 2014 na kocha Louis van Gaal.


Ungana nasi kupitia Facebook kwa ku like ukurasa wetu wa Kandanda 24 na tuffollow Twitter @Kandanda 24

Rooney: Sina tatizo na Sir Alex Ferguson Rooney: Sina tatizo na Sir Alex Ferguson Reviewed by Steve on Tuesday, September 08, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.