Propellerads

Nyota huyu wa Chelsea kuikosa mechi ya klabu bingwa kesho, pia kuna kikosi kitakachoanza



Chelsea kesho itacheza bila mshambuliaji wake Radamel Falcao
kwenye mechi ya kundi G michuano ya klabu bingwa dhidi ya Maccabi Tel Aviv.

Mchezaji huyo aliyepo kwa mkopo toka Monaco ana tatizo dogo na kutokuepo kwake kikosini huenda ikawa ni mechi moja pekee.

 Bosi wa Chelsea, Jose Mourinho amemzungumzia Mkolombia huyo na kusema ana tatizo dogo tu na hakuna cha zaidi.

"Hayumo kikosini. Alipata tatizo dogo mazoezini , sio muhimu sana. Haitakua muda mrefu sana, ni kwa mchezo huu pekee."

Mourinho aliongeza kwa kumzungumzia Oscar pia "Yuko fit kwa sababu hana majeraha.

Mlinda mlango Thibaut Courtois yupo nje kwa miezi mitatu kutokana na jeraha kwenye goti, kwa hiyo Asmir Begovic ataendelea kuwepo golini.

Kikosi kitakachoanza kwa Chelsea:
Begovic, Ivanovic, Fabregas, Zouma, Rahman, Oscar, Ramires, Hazard, Cuadrado, Mikel, Traore, Pedro, Remy, Costa, Matic, Willian, Cahill, Terry, Blackman, Azpilicueta, Loftus-Cheek, Kenedy, Beeney.

Nyota huyu wa Chelsea kuikosa mechi ya klabu bingwa kesho, pia kuna kikosi kitakachoanza Nyota huyu wa Chelsea kuikosa mechi ya klabu bingwa kesho, pia kuna kikosi kitakachoanza Reviewed by Steve on Tuesday, September 15, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.