Mastaa mbali mbali na mtazamo kuhusu nani mkali zaidi kati ya Messi na Ronaldo
Mjadala uliopo kwa muda mrefu sasa kua kati ya Ronaldo na Messi
nani mkali unaendelea ambapo mastaa Robin van Persie, David Luiz na Rio Ferdinand wametoa maoni yao.
Mastaa hao wametoa maoni yao katika mjadala ulioandaliwa na BT Sport ambapo kila mmoja katoa sababu kwanini anaona nani ni bora zaidi.
"Nimepata kucheza na Ronaldo, kwa hiyo siku zote namkubali sana." alisema Ferdinand
"Tofauti kati yao, kwangu ni kwamba Ronaldo anafunga magoli ya aina mbali mbali. Anaweza kufunga aina yoyote ya goli unavyoweza kufikiria-Ronaldo anafunga."
Beki wa Paris Saint-Germain, David Luiz yeye hakubaliani, anasema "Napendelea staili ya Messi, lakini Ronaldo yuko vizuri pia."
Aliyekua mshambuliaji wa Manchester United, Robin Van Persie yeye amesema ni swala gumu lakini amempa Messi.
"Ningependa kumpa Messi, lakini ni swala gumu sana." alisema.
Messi alishinda katika mjadala huo wa BT Sport kwa kura sita kwa tatu ambapo mastaa watatu (Ferdinand, Michael Owen na Owen Hargreaves) walimpa Ronaldo kama mchezaji waliyepata kucheza nae Man United.
"
Mastaa mbali mbali na mtazamo kuhusu nani mkali zaidi kati ya Messi na Ronaldo
Reviewed by Steve
on
Tuesday, September 15, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Tuesday, September 15, 2015
Rating:

No comments:
Post a Comment