Propellerads

Arsenal wathibitisha upasuaji wa Wilshere siku za hivi karibuni



Arsenal kupitia mtandao wao rasmi wamethibitisha kua
hivi karibuni mchezaji wake Jack Wilshere atafanyiwa upasuaji katika mfupa wa mguu wake wa kushoto na inaonekana anaweza kukaa nje kwa muda wa miezi mitatu.

Wilshere amekua akisumbuliwa na majeraha mara kwa mara siku za hivi karibuni ambapo ilisemekana anaweza kuwa nje kwa muda mrefu na sasa klabu wamelithibitisha hilo.

Ripoti kutoka mtandao wao zinasema wamechukua maamuzi hayo baada ya kupata ushauri kutoka kwa wataalamu kua jeraha la Wilshere sio la kupona mapema kama walivyotarajia.

Kwa kumfanyia upasuaji atakua nje kwa miezi mitatu ambapo kufikia Christmass huenda akawa amerejea uwanjani.

Hakuna shaka kua kwa majeraha yaliyomuandama utakua ni upasuaji mkubwa zaidi katika maisha yake ya soka.
Arsenal wathibitisha upasuaji wa Wilshere siku za hivi karibuni Arsenal wathibitisha upasuaji wa Wilshere siku za hivi karibuni Reviewed by Steve on Tuesday, September 15, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.