Propellerads

Kumbe ilikua kidogo tu Xavi aende Bayern ila Pep Guardiola akawa kikwazo




Aliyekua kiungo wa FC Barcelona, Xavi amefichua kua ilikua
ni kidogo tu ajiunge na Bayern Munich ya Ujerumani mwaka 2008 lakini kocha wake kipindi hicho Pep Guardiola alimwambia akatae kuhama.

Kiungo huyo anayekipiga Al-Sadd kwa sasa amefunguka kua bodi ya klabu ya Barca ilikua tayari kumuuza mwaka 2008 baada ya michuano ya Euro ambapo tayari Bayern walikua washampigia hesabu.

Lakini baada ya kuongea na Guardiola ambaye kwa wakati huo alikua amechaguliwa kua kocha wa Nou Camp,alijikuta akiishia kuendelea kubaki Catalunya.

"Baada ya Euro 2008, nilianza kuhisi kua Barcelona wako tayari kuniuza. Nilienda timu ya taifa nikijua klabu itakua tayari kuniuza kama ikija ofa nzuri" aliongea Xavi wakati alipokua katika interview na gazeti moja la kihispania liitwalo Marca.

"Niliongea na wakala wangu, Ivan Corretja, aliniambia kuna ofa kutoka Bayern,  Karl-Heinz Rummenigge ananihitaji.

"Baadae Guardiola akawa kocha mpya wa Barca na nilicheza vizuri sana kwenye fainali za Euro 2008. Pep akaniambia kua siwezi kwenda popote kwani nijaribu kufikiria Barcelona itakuaje bila uwepo wangu. Nilimwelewa kile alichosema."

Chini ya Guardiola, Xavi amepata kushinda mataji matatu ya La liga, mawili ya Copa del Reys, na mawili ya klabu bingwa.

Kumbe ilikua kidogo tu Xavi aende Bayern ila Pep Guardiola akawa kikwazo Kumbe ilikua kidogo tu Xavi aende Bayern ila Pep Guardiola akawa kikwazo Reviewed by Steve on Tuesday, September 15, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.