Propellerads

Uhuru Selemani arejea Dar kimya kimya, na hiki ndicho kimemleta




Mshambuliaji nyota wa Royal Eagles, Uhuru Selemani ametua jijini
Dar es Salaam, kimyakimya.

Uhuru amerejea nchini akitokea Afrika Kusini ikiwa ni siku chache baada ya kuifungia timu yake bao muhimu la ushindi dhidi ya Amazulu.

Uhuru aliifungia Royal Eagles bao katika ushindi wa mabao 2-1 ikiwa nchini mechi yake ya kwanza kucheza.

Awali, baada ya kuwepo kwa taarifa za kurejea kwake ilielezwa huenda amesigana na timu hiyo ya Afrika Kusini na alikuwa nchini kufanya mazungumzo na klabu moja kubwa hapa nchini.

Alipoulizwa sababu ya kurejea Dar es Salaam kimyakimya, Uhuru alisema ni masuala ya kifamilia.

“Ni masuala ya kifamilia lakini ndani ya siku moja mbili nitakuwa nimerejea kazini,” alisema.

“Kuna ishu ya vyeti vya watoto wangu nilitakiwa kuweka saini yangu, ni jambo muhimu. Hivyo nimerejea na nitaondoka.”





u
Uhuru Selemani arejea Dar kimya kimya, na hiki ndicho kimemleta Uhuru Selemani arejea Dar kimya kimya, na hiki ndicho kimemleta Reviewed by Steve on Tuesday, September 15, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.