Hii hapa sababu kutoka kwa uongozi kwanini Yanga hawakusema chochote kabla ya mechi na Simba
Kabla ya kuchezwa kwa mechi kati ya Simba na Yanga,
uongozi wa Yanga ulikaa kimya na haukuzungumza chochote hadi baada ya mchezo huo kuchezwa na kuibuka na ushindi wa goli 2-0.
Katibu mkuu wa Yanga Dr. Jonas Tiboroha ameeleza sababu za kukaa kimya mpaka mchezo huo dhidi ya watani wao wa jadi ulipochezwa.
“Kwenye medani ya mpira kama hii lazima watu wajifunze namna ya kuhimili presha za mpira, kitalamu mpira wa miguu haushindwi magazetini au maredioni. Kwamaana hiyo sisi tuliamua kujitoa pembeni hatukua mashabiki tulikuwa viongozi na ili uweze kuwa kiongozi lazima kuwe na ‘calmness’ ili uweze kuplan mambo yako na na namna gani game itachezwa na vitu kama hivyo”, amesema Dr. Tiboroha.
“Sasa wenzetu waliamua kuwa mashabiki wakaamua kukaa na kupiga makelele magazetini lakini ukumbuke hii ni ‘secretariat’ mpya imeingia, toka tumeingia sisi tumefungwa na Simba mechi moja na kusema ukweli, tulijifunza mambo mengi siku ile”.
“Ni kutokana na mambo tuliyojifunza kipindi kile, tuliamua kuja na mikakati mipya na nikwambie kitu kimoja, usitegemee sasahivi tutakapokuwa tunacheza mechi yoyote kutusikia sisi tunaongea magazetini”.
Hii hapa sababu kutoka kwa uongozi kwanini Yanga hawakusema chochote kabla ya mechi na Simba
Reviewed by Steve
on
Tuesday, September 29, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Tuesday, September 29, 2015
Rating:

No comments:
Post a Comment