Hat trick aliyopiga Sanchez dhidi ya Leicester jana, Wenger amesema hivi
Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger amempa sifa Alexis Sanchez
kwa kukubali kua nyota huyo anafaa kuitwa 'world class' baada ya kutupia hat trick jana dhidi ya Leicester.
Forward huyo kutoka Chile hakua amezifuma nyavu tangu Mei 4 walipoifunga Hull City 3-1. Lakini jana walipokutana na vijana wa Claudio Ranieri alitupia zake tatu zote kwa mashuti.
Wenger aliulizwa na Sky Sports kwamba Sanchez anaweza kuitwa 'world class'- neno ambalo limesikika sana wiki hii baada ya Sir Alex Ferguson kutaja wachezaji wanne wa aina hiyo aliopata kuwafundisha.
Wenger alijibu "Nadhani ni hivyo"
"Nadhani nina wachezaji wengi ambao ni world class. Unatakiwa uelewe maana ya hii lakini yote kwa yote (Sanchez) ni mshambuliaji mwenye hamasa na anayejituma kwa ajili ya timu. Kama timu ikicheza vizuri anaweza kufunga magoli."
Magoli mengine ya Arsenal yalifungwa na Walcott na Giroud hivyo kuipa Arsenal matokeo ya 5-2 mbele ya Leicester ambao magoli yao nao yalifungwa na Vardy na Drinkwater.
Pia katika mechi nyingine EPL zilizochezwa jana matokeo yalikua hivi
Spurs 4-1 Man City
Leicester 2-5 Arsenal
Liverpool 3-2 Aston Villa
Man Utd 3-0 Sunderland
Southampton 3-1 Swansea
Stoke 2-1 Bournemouth
West Ham 2-2 Norwich
Newcastle 2-2 Chelsea
Hat trick aliyopiga Sanchez dhidi ya Leicester jana, Wenger amesema hivi
Reviewed by Steve
on
Sunday, September 27, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Sunday, September 27, 2015
Rating:

No comments:
Post a Comment