Hans Poppe asema yeye tayari ashakamilisha kazi yake
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe
amesema amemaliza kazi yake na ameishakabidhi mikoba kwa kamati nyingine.
Akizungumza na mtandao wa SALEHJEMBE, Hans Poppe amesema kuwa baada ya kukamilisha usajili, amekabidhi kila kitu kwa kamati ya ufundi na ile ya mashindano.
“Kazi ya kamati ya usajili imeisha, tumeishakabidhi kila kitu kwa kamati ya ufundi na ile ya mashindano.
“Tunachosubiri sasa ni kuanza kwa ligi, hapo tunaweza tukawa tunaangalia mambo mbalimbali ya kufanya na nini tusaidie,” alisema Hans Poppe.
Simba ni kati ya timu zilizofanya usajili mkubwa kwa ajili ya msimu ujao na sasa inachosubiri ni kuanza tu kwa ligi.
ngana nasi kupitia Facebook kwa ku like ukurasa wetu wa Kandanda 24 na tuffollow Twitter @Kandanda 24
Hans Poppe asema yeye tayari ashakamilisha kazi yake
Reviewed by Steve
on
Tuesday, September 08, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Tuesday, September 08, 2015
Rating:

No comments:
Post a Comment