Suarez amefichua siri ya uhusiano kati yake na Messi na Neymar
Luis Suarez amefichua siri ya uhusiano iliyopo kati yake
yeye, Messi na Neymar.
Combination hiyo ya ushambuliaji pia ni maarufu kama MSN ambapo mwaka jana walivunja rekodi ya magoli 122 waliyofunga pamoja.
Suarez amesema siri ya uhusiano wao imara inatokana na kutokua na wivu kati yao ila kubwa kabisa wana lengo la kuipa mafanikio klabu .
"Tuna lengo moja-kuipa Barca vikombe. Uhusiano ni mzuri sana ndani na nje ya uwanja" aliiambia La Vanguardia.
"Wote tunajua kua Leo(Messi) ni bora. Hakuna kati yetu anayetaka kujaribu kumzidi au kuwa sawa na alipo.
"Hakuna wivu. Sisi ni sehemu ya timu, na hatuna lengo la kushindana kati yetu"
Suarez alifunga magoli 25 msimu uliopita Cmp Nou na kutoa usaidizi mara 14 japokua alianza kucheza amechelewa kidogo kutokana na kutumikia adhabu aliyokua amepewa na FIFA.
Ungana nasi kupitia Facebook kwa ku like ukurasa wetu wa Kandanda 24 na tuffollow Twitter @Kandanda 24
Suarez amefichua siri ya uhusiano kati yake na Messi na Neymar
Reviewed by Steve
on
Wednesday, September 09, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Wednesday, September 09, 2015
Rating:

No comments:
Post a Comment