Cheki huyu aliyemtabiria Martial wa Man United kutisha kama Thierry Henry
Louis Saha amemtabiria nyota mpya wa Man United,
Antony Martial kua atafanya makubwa kama ilivyokua kwa Thierry Henry alipokua Arsenal.
Martial aliweka rekodi ya kua mchezaji ghali zaidi kwa vijana jumanne iliyopita baada kusajiliwa na Man United kutoka Monaco kwa dau la thamani ya £36m ambalo inadaiwa linaweza kupanda na kufikia £58m.
Tayari nyota huyo amefananishwa na nyota mwenye rekodi kubwa ya ufungaji Arsenal, Thierry Henry huku Saha akisema dogo huyo ana uwezo wa kuleta balaa ligi ya England.
"Ana kasi, nguvu, na pia nikijana ataleta mshangao kwa mabeki wengi kwa sababu hawamjui vizuri" Saha alinukuliwa na Goal.com "NI asset kubwa kwa Man United na hicho ndicho walihitaji kwa sababu mbele muda mwingine walikosa kasi.
"Ufaransa tunamuita Thierry Henry anayefatia kwa sababu anaweza kucheza kulia au kushoto, ana uwezo mkubwa wa kukaa na mpira na anaweza kuwakimbiza mabeki kuanzia watatu, wanne, hakuna tataizo. Hapo hapo hana hofu.
"Ana uwezo wa kuchukua mataji mengi na Man United, lakini hilo nisilipe msukumo sana"
Martial alianzia kuchezea klabu ya mtaani ya Les Ulis ambayo ndio hiyo hiyo iliyomtoa Thierry
Henry.Ungana nasi kupitia Facebook kwa ku like ukurasa wetu wa Kandanda 24 na Twitter @Kandanda 24
Cheki huyu aliyemtabiria Martial wa Man United kutisha kama Thierry Henry
Reviewed by Steve
on
Monday, September 07, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Monday, September 07, 2015
Rating:

No comments:
Post a Comment