Kumbe hiki ndio kilimsaidia Kapombe kung'aa game ya Nigeria!!
Baada ya beki wa kulia wa Taifa Stars, Shomari Kapombe
kuonyesha soka maridadi juzi Jumamosi na kufanikiwa kuwadhibiti washambuliaji wa Nigeria, hasa staa wa KAA Gent ya Ubelgiji, Moses Simon, amefunguka kuwa kilichomsaidia ni akili nyingi tu, wala si kingine.
Katika mchezo wa juzi Jumamosi kufuzu Afcon 2017, Kapombe alionekana kuwa makini muda wote na kufanikiwa kudhibiti mashambulizi ya hatari yaliyotaka kuundwa kutokea upande wake kupitia kwa winga Moses kabla ya winga huyo kuonekana kufeli na kocha wake, Sunday Oliseh kuamua kumtoa kwenye dakika ya 69 na kumuingiza Edouk Samuel.
“Unajua kilichotokea pale ni kugundua unahitaji kutumia nini kwa mshambuliaji kama yule, yeye anatoka kwenye ligi za kimataifa na ashakutana na changamoto ya mabeki wengi wazuri, kwa hiyo ana changamoto ya kutosha, kilichohitajika ni umakini mkubwa juu yake na kucheza kwa akili kubwa.
“Hiyo ndiyo ilikuwa silaha yangu, nilimchezea kwa akili sana lakini pia ujanja na mbinu tulizopewa na kocha Mkwasa (Boniface) zilisaidia kujiamini na kucheza vile, ndiyo maana unaona safu yetu ya ulinzi kwa ujumla ilitulia, nafikiri ni mwanzo mzuri, kila mmoja ameona kazi ilivyokuwa, tunaomba Watanzania waendelee kutusapoti,” alisema Kapombe.
Henry.Ungana nasi kupitia Facebook kwa ku like ukurasa wetu wa Kandanda 24 na Twitter @Kandanda 24
Kumbe hiki ndio kilimsaidia Kapombe kung'aa game ya Nigeria!!
Reviewed by Steve
on
Monday, September 07, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Monday, September 07, 2015
Rating:

No comments:
Post a Comment