Propellerads

Busungu aamua kusikiliza ushauri wa Pluijm kisha akaamua haya



Mshambuliaji mpya wa Yanga, Malimi Busungu, amejikuta
akishinda chumbani kwake muda mwingi akitafakari maelezo ya kocha wake, Hans van Der Pluijm ambaye amemtaka kujifunza kupambana na kutokata tamaa.

Azam wao hawatatumia jezi za wadhamini wa ligi Vodacom, ijue sababu hapa

Busungu amefikia hatua hiyo baada ya kuonekana kukata tamaa kutokana na ushindani mkali wa namba uliopo kikosini hapo.

Pluijm aliamua kumpa darasa kubwa mchezaji huyo ambaye ametua Yanga hivi karibuni akitokea Mgambo ya Tanga, baada ya kuona makali yake yanapotea.
 Busungu alisema: “Aliniambia mambo mengi sana na mengine kwa faida yangu lakini kikubwa alikuwa akinitaka niongeze bidii mazoezini kwani ana imani na mimi, pia nisisikilize maneno ya watu wa nje ambayo wamekuwa wakisema juu yangu.

“Hakika hali hiyo ilinifanya nitumie muda mwingi baada ya mazoezi nikiwa chumbani kwangu nikitafakari moja baada ya jingine, kusema kweli Pluijm ni bonge la kocha na sasa najiona kama nimezaliwa upya, hivyo ngoja ligi ianze.”

Ungana nasi kupitia Facebook kwa ku like ukurasa wetu wa Kandanda 24 na Twitter @Kandanda 24

Busungu aamua kusikiliza ushauri wa Pluijm kisha akaamua haya Busungu aamua kusikiliza ushauri wa Pluijm kisha akaamua haya Reviewed by Steve on Friday, September 04, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.