Azam wao hawatatumia jezi za wadhamini wa ligi Vodacom, ijue sababu hapa
Timu za Ligi Kuu Bara zilikabidhiwa jezi na vifaa kutoka
kwa wadhamini wa michuano hiyo, Kampuni ya Vodacom, juzi, lakini imebainika kuwa Azam FC haitavitumia.
Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba, amesema timu yake imekuwa ikifanya hivyo kwa misimu kadhaa.
Ingawa hakutoa sababu za kina juu ya maamuzi yao hayo lakini alifunguka hivi:
“Huwa hatuzitumii hizo jezi, msimu wa pili sasa tunatumia jezi zetu wenyewe, cha msingi ni kufuata utaratibu unavyotakiwa, kama vile kuwepo kwa nembo ya mdhamini kwenye sehemu husika ya jezi na mambo mengine, ndiyo maana tunatumia za kwetu wenyewe na hakuna tatizo.
“Zile jezi tunazopewa na mdhamini mara kadhaa huwa tunazigawa kwa timu zetu za vijana au kwingine, hata zile za mazoezi kama bips tunazopewa pia hatuzitumii, tunatumia tunazotengeneza wenyewe na ni kwa sababu tunapenda zaidi kutumia vya kwetu wenyewe.”
Ungana nasi kupitia Facebook kwa ku like ukurasa wetu wa Kandanda 24 na Twitter @Kandanda 24
Azam wao hawatatumia jezi za wadhamini wa ligi Vodacom, ijue sababu hapa
Reviewed by Steve
on
Friday, September 04, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Friday, September 04, 2015
Rating:




No comments:
Post a Comment