Propellerads

Wakala: Chelsea wanaweza kumsajili Pogba mwezi Januari



Imeripotiwa kua Chelsea wanaweza kuipata
saini ya Pogba mwezi januari mwakani, hii ni kwa mujibu wa wakala wa soka  Mesrin Izzet.

Chelsea mara kwa mara katika kipindi cha joto wamehusishwa sana na Pogba lakini hakukufanyika dili lolote.



Matokeo yake kiungo John Obi Mikel alizuiwa kuondoka kuelekea  Besiktas  pamoja na kwamba aliripotiwa kukaribia kukamilisha dili hilo.

Hata hivyo wakala Izzet amedai kua Obi Mikel ameshafanya makubaliano na klabu hiyo ya Uturuki, lakini dili hilo litakamilika endapo Chelsea wataipata saini ya Pogba katika dirisha lijalo la usajili.

"Chelsea wanaweza kumsainisha Pogba kipindi dirisha la usjili likifunguliwa tena na hii itafungua mlango wa Mikel kusaini na Bestikas" Izzet aliiambia redio moja ya michezo  Radyospor ya Uturuki.

"Mikel ameniambia kua anataka kucheza Uturuki kwa sababu anahitaji zaidi kuanza na kikosi cha kwanza cha timu ambapo bado haijawa baada ya Mourinho kuitosa dili ya Bestikasi"

Ungana nasi kupitia Facebook kwa ku like ukurasa wetu wa Kandanda 24 na Twitter @Kandanda 24


Wakala: Chelsea wanaweza kumsajili Pogba mwezi Januari Wakala: Chelsea wanaweza kumsajili Pogba mwezi Januari Reviewed by Steve on Friday, September 04, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.