David Luiz alivyofunguka kuhusu kuhama kwake Chelsea
David Luiz amesisitiza kua aliamua mwenyewe
kuondoka Chelsea na sio kwamba kocha Jose Mourinho ndio aliamua.
Mbrazili huyo aliondoka Stamford Bridge na kuelekea PSG majira yaliyopita katika kombe la dunia kwa ada ya pauni mil 50.
Luiz ameeleza kua hakua na mawasiliano sana na Mourinho kabla ya kutimka.
"Kilikua ni kipindi ambacho nilijifunza mengi. Nisingeweza kusema kilikua kigumu" aliiambia Bleacher Report.
"Ukiishi katika mazingira na hali tofauti katika maisha yako, nilijua nitaondoka kabla hata ya kombe la dunia.
"Kipindi nilipoondoka, nilikua na timu ya Brazili, na sikua na mawasiliano yoyote nae (Jose Mourinho). Kwanza nilikua mapumzikoni Brazil kisha kombe la dunia.
"Kila kilicholetwa kwangu nilikubali, na alinitumia ujumbe mdogo ukisema 'good luck'. Baada ya hapo nilienda moja kwa moja Paris, sikurudi tena London".
Luiz aliichezea Chelsea mechi 143 katika michuano yote.
Ungana nasi kupitia Facebook kwa ku like ukurasa wetu wa Kandanda 24 na Twitter @Kandanda 24
David Luiz alivyofunguka kuhusu kuhama kwake Chelsea
Reviewed by Steve
on
Friday, September 04, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Friday, September 04, 2015
Rating:




No comments:
Post a Comment