Cheki Pedro alivyomkandia Van Gaal juu ya kina Valdes, De Gea
Pedro amefunguka maoni yake juu ya vitendo vya
kocha wa Man United Louis van Gaal kwa kina David De Gea na Victor Valdes kua havikua vya haki.
Walinda mlango hao wote walikua katika kizungumkuti cha kutaka kuondoka Man United, ambapo van Gaal alianza kwa Valdes kumwambia kua klabu haina mpango nae tena, huku De Gea nae akiwa hajacheza mpaka sasa kutrokana na swala lake la kwenda Real Madrid.
Kabla ya kujiunga Chelsea mwezi uliopita, Pedro alihusishwa kujiunga na Man United lakini amekanusha kua kutopendezwa na mambo ya kocha van Gaal sio sababu ya kukataa ofa ya United
Alipoulizwa kua vitendo vya kocha Van Gaal kwa wahispania wenzake ndio sababu ya yeye kususia ofa ya Red Devils, Pedro alijibu "Hapana.
"Ni kweli sikufurahishwa na mambo waliyokua wakifanyiwa wenzangu, hasa Victor ambaye namchukulia kama teammate mwenzangu na pia professional.
"Siamini kama ni vizuri, lakini haikushawishi maamuzi yangu.
Hispania wataumana na Slovakia jumamosi hii katika kufuzu Euro 2016.
Cheki Pedro alivyomkandia Van Gaal juu ya kina Valdes, De Gea
Reviewed by Steve
on
Thursday, September 03, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Thursday, September 03, 2015
Rating:




No comments:
Post a Comment