Propellerads

Alex Ferguson afichua sababu iliyomfanya ang'atuke Man United




Aliyekua meneja mkongwe wa Man United, Sir Alex Ferguson
amefunguka kua angekua bado anafundisha soka kama isingekua matatizo ya kifamilia mwaka 2012.

Kocha huyo mskochi alistaafu mwaka 2013 ambapo amefichua kua kifo cha pacha wa mke wake ndio sababu kubwa ya yeye kuamua hivyo.

"Ningeweza kuendelea" aliiambia The Telegraph

"Nilimwona (Mke wake Cathy) akiangalia TV usiku mmoja, huku akiangalia juu ya dari. Nikajua yuko mpweke sana. Yeye na Bridget walikua mapacha unajua?"

Ferguson katika wakati wake wa miaka 27 Man United ameshinda mataji makubwa 25-  yakiwemoya Premier League 13, mawili ya Champions League

Red Devils tangu kuondoka kwa kocha huyo hawajachukua taji lolote kubwa.

Alex Ferguson afichua sababu iliyomfanya ang'atuke Man United Alex Ferguson afichua sababu iliyomfanya ang'atuke Man United Reviewed by Steve on Saturday, September 19, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.