Uvumi wa kuhamia Man United, Bale mwenyewe afunguka hivi
Nyota Gareth Bale amesisitiza mwenyewe kua ana hamu na anaweza kupata
mafanikio makubwa zaidi Real Madrid, ameyasema hayo kufuatia uvumi wa muda mrefu wa kuhusishwa na kuhamia Red Devils ambao wamekua wakiripotiwa kumtengea ofa kubwa.
Jumanne iliripotiwa kua Man United wameweka ofa mbili kwa zaidi ya pauni 100m kwa nyota huyo ambaye uhamisho wake akitokea Tottenham kwenda Real ulivunja rekodi kwa pauni 85m.
Bale, msimu uliopita hakua katika kiwango chake, hali iliyopelekea wengi kudai labda huenda angerudi tena England.
"Ninajiamini, ni jambo kubwa kupata support kutoka kwa kocha na pia rais wa klabu,na nina matumaini nitawalipa kwa magoli na mataji" Bale aliwaambia waandishi Hispania.
Bale, ambae mkataba wake ma Real unaisha mwaka 2019, alipata kufunga kwenye mechi ambayo walishinda 2-0 dhidi ya Tottenham katika kombe la Audi.
Uvumi wa kuhamia Man United, Bale mwenyewe afunguka hivi
Reviewed by Steve
on
Wednesday, August 05, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Wednesday, August 05, 2015
Rating:

No comments:
Post a Comment