Mourinho ashindwa kuhudhuria mkutano wa makocha, sababu inaweza kua ni Wenger!!?
Kocha Jose Mourinho wa Chelsea hakuhudhuria mkutano wa makocha jana ambapo
pia mkutano huo ulihudhuriwa na Arsene Wenger.
Bosi huyo wa Chelsea yuko katika uhasama na Wenger baada ya kutopeana mikono katika mechi ya ngao ya jamii ambapo Arsenal walishinda 1-0.
Wenger aliingia mkutanoni hapo uliofanyikia makao makuu ya Premier League huko Gloucester Place, London, pamoja na makocha wengine.
Lakini Mourinho hakuonekana wala mwakilishi yeyote wa benchi la ufundi kutoka Chelsea na hakukua na sababu yeyote ya udhuru.
Hali hii ilipelekea mtendaji wa Premier League kuwasihi makocha kutoacha kuja mkutano huu muhimu.
Makocha wengine wa vilabu vikubwa kama vile Louis van Gaal walikuwepo katika tukio hilo ambapo huzungumzia mambo mbalimbali kujiandaa na msimu mpya wa ligi.
Mourinho ashindwa kuhudhuria mkutano wa makocha, sababu inaweza kua ni Wenger!!?
Reviewed by Steve
on
Wednesday, August 05, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Wednesday, August 05, 2015
Rating:





No comments:
Post a Comment