Propellerads

Ramos amewachomolea Real Madrid, je anatua Man United!?...jibu lipo hapa




Imeripotiwa kua nyota Sergio Ramos amekataa kuongeza mkataba mpya na
klabu yake ya Real Madrid, na hii inaweza kua taarifa njema kwao Manchester United.

Jahazi la Tanzania katika soka linazidi kuzama, nani wa kuliokoa!!

Nyota huyo mhispania katika kipindi hiki cha usajili amehusishwa sana kuhamia Red Devils, lakini wiki iliyopita matumaini ya kocha van Gaal kunasa saini ya mkali huyo yaliyeyuka ghafla baada ya kupatikana taarifa kua anaongeza mkataba wake na Real Madrid.

Sasa taarifa mpya zimepatikana kupitia gazeti la Kihispania, AS limedai kua mazungumzo ya mkataba mpya kati ya Real na nyota huyo yamevunjika baada ya ofa ya kiasi cha  £5.6m kwa mwaka kukataliwa na Ramos.

Ripoti zinadai Ramos anataka kiasi cha  £7m kwa mwaka katika mkataba huo, na kukosekana maendeleo yoyote katika mazungumzo hayo  Man United wanaweza kumnasa kabla ya dirisha la usajili kufungwa.


Ramos amewachomolea Real Madrid, je anatua Man United!?...jibu lipo hapa Ramos amewachomolea Real Madrid, je anatua Man United!?...jibu lipo hapa Reviewed by Steve on Friday, August 07, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.