John Terry amepigwa 'beat' na Martinez kuhusu John Stones
Kocha wa Everton, Roberto Martinez amemuonya nyota wa
Chelsea, John Terry kutozungumzia wala kujihusisha kwa lolote katika ishu ya usajili wa John Stones.
Jahazi la Tanzania katika soka linazidi kuzama, nani wa kuliokoa!!
Hali hii inafuatia Terry kufunguka hadharani kua anaamini usajili wa John Stones utakua ni wa nguvu sana kwa Chelsea- kitendo ambacho Martinez ametafsiri kua sio halali.
Martinez kama alivyonukuliwa na The Mirror amesema "Unajua hii sio halali, sheria hazikuruhusu kuongelea wachezaji waliosajiliwa vilabu vingine katika hali ya uwazi hivyo, imenisikitisha.
"Unajua, najua. Na wote tunafahamu kuna sheria na miongozo ni kitu ambacho hatupendi kusikia vilabu vingine vikioongelea wachezaji wetu, sio sahihi na haitakiwi itokee"
Huku hayo yakitokea, tayari The Blues walishatuma ofa mbili kwa Everton ili kumnasa John Stones lakini zote zikakataliwa na Martinez, kocha Mourinho bado ana matumaini ya kumnasa beki huyo.
John Terry amepigwa 'beat' na Martinez kuhusu John Stones
Reviewed by Steve
on
Friday, August 07, 2015
Rating:
No comments:
Post a Comment