Kufuatia sare na Swansea, Mourinho atupa lawama kwa madaktari
Kocha Jose Mourinho amewakosoa madaktari wa timu yake kwa
'kutoelewa' na kumpa matibabu Hazard kwenye mechi ya jana ambayo walitoa sare ya 2-2 na Swansea.
Kipa wa The Blues, Thibaut Courtois alitolewa kwa kadi nyekundu hali iliyopelekea wachezaji wakabaki kumi , Hazard nae alipotolewa nje kwa matibabu pamoja na kwamba hakuumia sana, wachezaji walibaki tisa pekee
Kama mchezaji akiwa anatibiwa, lazima atolewe nje ya uwanja kwanza. Sasa kitendo hiki kimemuudhi Mourinho hadi kuwalaumu wafanyakazi wake wa afya.
"Staff wa afya hawajanifurahisha, kwani hawakua wajanja na wasiojua" Mourinho aliiambia Sky Sports
"Ukiwa kit man, daktari au katibu kwenye benchi unatakiwa uuelewe mchezo.
"Unatakiwa kuelewa kua kuna upungufu wa mchezaji mmoja. Ili kumsaidia mchezaji unatakiwa kujua kama ana tatizo kubwa. Najua Hazard hakua na tatizo kubwa, alipata mshtuko. Alikua amechoka"
Chelsea tayari walikua pungufu baada ya kutolewa kwa Kipa Courtois, lakini pia baada ya Hazard kutolewa kwa matibabu kulimchanganya zaidi Mourinho.
Courtois alipewa kadi nyekundu baada ya kumwangusha mshambuliaji wa Swansea Bafetimbi Gomis katika dakika ya 52, lakini Mourinho amekataa kuizungumzia kadi hiyo na kudai ni maamuzi ya mwamuzi.
Kufuatia sare na Swansea, Mourinho atupa lawama kwa madaktari
Reviewed by Steve
on
Sunday, August 09, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Sunday, August 09, 2015
Rating:



No comments:
Post a Comment