Propellerads

Baada ya mchezo wa jana, van Gaal ameongea kuhusu kiwango cha Depay




Bosi wa Man United, Louis van Gaal amefunguka kua haoni shida yoyote katika
kiwango alichoonesha nyota Memphis Depay kwenye mchezo wa jana dhidi ya Tottenham.

Depay alionekana kujitahidi kuonesha madhara yake bila mafanikio kwenye mchezo huo ambapo Man United waliibuka na ushindi wa 1-0 lakini van Gaal amemtetea na kudai kua anaamini muda si mrefu atayazoea maisha ya Premier League.

BBC Sport wamemnukuu van Gaal akisema "Nilimwambia Memphis asicheze kwa hamu sana, lakini hivi ndivyo inavyokua katika siku za mwanzo kucheza Old Trafford, hua ni vigumu sana"

Nyota huyo mwenye miaka 21 aliifungia PSV magoli 50 katika mechi 124.
Baada ya mchezo wa jana, van Gaal ameongea kuhusu kiwango cha Depay Baada ya mchezo wa jana, van Gaal ameongea kuhusu kiwango cha Depay Reviewed by Steve on Sunday, August 09, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.