Tetesi: Man United kumtumia Evans kumnasa John Stones
Manchester United wanajaribu kumnasa beki wa Everton ambae pia anawindwa na
Chelsea, John Stones, huku ikidaiwa Johnny Evans atatumika katika kufanikisha dili hiyo.
Stones amekua akihusishwa kutaka kuondoka Everton msimu huu, huku Chelsea wakihusishwa nae ambapo mpaka sasa madau yao mawili yamekataliwa.
Hata hivyonaonekana kama kuna vita kuinasa saini ya beki huyo kwani kwa mujibu wa The Mirror ,
ambao wanadai Mbali ya Chelsea na Man United, Man City pia nao wanadaiwa kumtaka.
Everton walihusishwa kumtaka Evans, kwa hiyo Man United wanaweza kutumia nafasi hiyo kama chambo ya kumnasa John Stones ingawa mpaka sasa Everton wamesisitiza hawamuuzi.
Tetesi: Man United kumtumia Evans kumnasa John Stones
Reviewed by Steve
on
Friday, July 31, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Friday, July 31, 2015
Rating:

No comments:
Post a Comment