Jerry Muro anasaka kupitishwa kugombea ubunge kupitia CCM
Uchaguzi mkuu wa Tanzania wa Rais, Wabunge na Madiwani unatarajia kufanyika Oktoba mwaka huu na
tayari watu wenye nia ya kugombea wameanza kuwashawishi wanachama wa vyama vyao.
Tofauti na miaka mingine, mwaka huu watu wa aina mbalimbali wamejitokeza wakiwemo waandishi wa habari, wasanii tena vijana kabisa.
Mkuu wa Idara ya habari na Mawasiliano wa Yanga, Jerry Muro ‘Wakimataifa’ amejitoka kusaka nafasi ya kugombea Ubunge katika jimbo la Kawe, Dar es salaam kupitia Chama Cha Mapinduzi.
Muro na watangaza nia wenzake wanamwaga sera kwa wanachama wa CCM ili kuteuliwa kugombea.
Swali linabaki pale pale. Jerry Muro atakatwa au hatakatwa na Wanachama wa CCM?..Tusubiri dakika 90 za siasa….
Jerry Muro anasaka kupitishwa kugombea ubunge kupitia CCM
Reviewed by Steve
on
Friday, July 31, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Friday, July 31, 2015
Rating:


No comments:
Post a Comment