Propellerads

Okwi ndani ya Denmark alivyotambulishwa rasmi.



Mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Simba na timu ya taifa ya Uganda ‘The Cranes’ Emanuel Okwi amekamilisha
uhamisho wake wa kujiunga na klabu yake mpya ya Sønderjysk ya Denmark na amesaini mkataba wa miaka minne kuitumikia klabu hiyo baada ya kufuzu vipimo vya afya.
Klabu ya Sonderjyske ya nchini Denmark imemkaribisha mshambuliaji wake mpya, Raia wa Uganda,  Emmanuel Okwi na kumkabidhi jezi yake namba 25 ambayo alikuwa anaitumia alipokuwa anacheza Simba.


Mkurugenzi wa michezo wa klabu hiyo Hans Jørgen Haysen amesema, wamekuwa wakimfuatilia Okwi na wamefurahi kumsaini mshambuliaji huyo. “Tumekuwa tunamfuatilia Emanuel Okwi kwa muda sasa, na tumefurahi tumefanikiwa kukubaliana nae, si yeye tu bali hata klabu yake ya zamani Simba SC kwa kukubaliana nasi”, Jørgen aliiambia tovuti ya klabu.
Hans Jørgen amesema, Okwi atatoa mbadala kwenye timu hasa kwenye eneo la ushambuliaji na wanatarajia makubwa kutoka kwake lakini akasema mshambuliaji huyo anaweza akahitaji muda kidogo ili kuendana na soka la Ulaya.
“Tukiwa na Emanuel Okwi, tutakuwa na uwanda mpana wa kucheza vizuri kwenye eneo la ushambuliaji na ni mchezaji ambaye tunatarajia mengi sana kutoka kwake”, Hans Jørgen amesema.
“Tunaamini atadumu kwa muda mrefu na kutengezeza jina kubwa kwenye Alka Super League, ingawa tunaelewa kwamba atahitaji muda ili kuendana na soka la Ulaya”, alimaliza.
Okwi ndani ya Denmark alivyotambulishwa rasmi. Okwi ndani ya Denmark alivyotambulishwa rasmi. Reviewed by Steve on Friday, July 10, 2015 Rating: 5
Propellerads
Powered by Blogger.