Propellerads

Tetesi za usajili Ulaya leo Ijumaa.






Tetesi: Man Utd na PSG wamekubaliana dili la pauni mil. 45 kwa Di Maria.
\\\\\\\\\UKulingana na ripoti kutoka Ufaransa zinadai Man Utd na PSG wamekubaliana
kiasi hicho cha pesa kwa ajili ya Di Maria. Pia ripoti zinazidi kudai Di Maria mwenyewe tayari ameshafanya mazungumzo binafsi na PSG na atakua miongoni mwa nyota wanaolipwa zaidi klabuni hapo, lakini dili linaweza kukamilika mpaka mwishoni mwa mwezi huu July.

Real wamekata tamaa kwa Otamendi
Real Madrid wanadaiwa kukata tamaa na mpango wa kumnasa Nicolas Otamendi kwani wanaamini kua nyota huyo tayari ana nafasi kubwa ya kuelekea Man United, Otamendi aliliripotiwa kua na makubaliano na mashetani hao wekundu, lakini hata hivyo Real wanajaribu kuwaomba Valencia wawapunguzie bei ya sasa ( pauni mil 35)

Wadhamini wa Real Madrid wathibitisha kutimia dili la Casillas
Kupitia tweet yao, Bwin wamethibitisha kuondoka kwa Casillas kwani wamesema kutakua na sherehe kubwa Ijumaa (leo) jioni kwa ajili ya kumuaga. Kama akienda Porto, Casillas atakua mwanasoka anaelipwa zaidi Ureno.

Schweinsteiger avutiwa na Man United
Nyota huyu amevutiwa na dili la Man united, kwa mujibu wa mwenyekiti wa klabu ya Bayern, Karl-Heinz Rummenige. Bosi huyo aliongea na Bastian kwenye simu huku wakitarajia kua na mazungumzo na nyota huyo akitoka mapumzikoni.

Sterling anataka kwenda Man City??
Raheem Sterling anaripotiwa kutohudhuria mazoezi ya klabu yake ya Liverpool kwa siku ya pili sasa huku akidai mgonjwa, lakini inasemekana ni kama njia ya yeye kushawishi kwenda Man City ambao wanataka kumsajili kwa pesa inayozidi pauni mil. 35.

Darmian kuchukua vipimo vya afya Man United
Beki wa kulia kutoka Italia, Matteo Darmian ameripotiwa kutua muda wowote leo jijini Manchester kwa ajili ya vipimo vya afya, hii ni kwa mujibu wa ripoti kutoka nchini Italia. Nae kocha wa Torino, Giampiero Ventura amethibitisha taarifa hizo, huku akimtakia Darmian kila la heri katika dili lake hilo la pauni mil. 13


Tetesi za usajili Ulaya leo Ijumaa. Tetesi za usajili Ulaya leo Ijumaa. Reviewed by Steve on Friday, July 10, 2015 Rating: 5
Propellerads
Powered by Blogger.