Usajili wa Mbuyu Twite, Yanga wanena haya.
Baada ya mchezaji wa Yanga Mbuyu Twite kuongeza mkataba mwingine mpya wa kuendelea kusalia kwenye
kikosi hicho, viongozi wa klabu ya FC Lupopo (klabu aliyokuwa akiichezea zamani Twite) wakaamua kuja kudai pesa wakisema Yanga wako nje ya makubaliano yao ya awali. Klabu ya Yanga kupitia kwa katibu wake mkuu wamelitolea ufafanuzi jambo hilo.
Katibu mkuu wa Yanga Dkt. Jonas Tiboroha amesema, kilakitu kilishamalizika tangu mwaka jana lakini kwavile viongozi wa FC Lupopo walikuwa hawajaelewa vizuri mkataba, tayari wamesha yaongea mambo hayo vizuri na viongozi hao wanaonekana kuelewa vizuri.
“Kilichonishangaza ‘this time’ ni kwamba hiyo ‘ishu’ ilishakuwa ‘sorted’ mwaka jana, na kwanza nikupongeze umeipataje hii taarifa, nikwambie tu Yanga mwaka jana walishafikia muafaka na FC Lupopo walipofanya maongezi na rais wa FC Lupopo Bw. Kasongo na walikubaliana Yanga watoe kiasi ambacho walikitoa mwaka jana ili iweze kumsajili Mbuyu Twite kwa miaka miwili”, amesema.
“Mwaka jana Twite alikuwa asaini miaka miwili, lakini Yanga baada ya kuwa tumefanya makubaliano ilikuwa imemsajili Mbuyu Twite kwa mwaka mmoja, sasa kilichowashangaza ni kusikia Mbuyu Twite mwaka huun ame-extend mkataba wake kwa mwaka mwingine wao wakaamua kuja kudai hela, kwa bahati nzuri walipofika mimi nikaingia kwenye mafaili nikawaonesha vitu kilichonishangaza pia wao wanalalamika kuwa yale makubaliano walikuwa hawajayapata japokuwa walipokea hela na hicho kitu kilinishangaza kidogo kwamba wamepokea pesa bila kujua mkataba wowote waliotumiwa”, amefafanua.
“Lakini nafikiri haya mambo tumeyaongea vizuri jana wamekaa na wanaonekana kuelewa, kikao cha mwisho tunakifanya kesho asubuhi (leo)”, ameeleza.
Alipoulizwa juu ya usajili wa golikipa wa KMKM ambapo Yanga walishindwana na klabu hiyo ya KMKM lakini baadae KMKM wakataka kupunguza ada ya uhamisho na timu hizo zikalazimika kukaa tena mezani, Tiboroha akasema, suala hilo bado lipo jikoni na watalizungumza Jumatatu au Jumanne.
“Hii naomba kwanza tusiiongelee tutaiongea Jumatatu au Jumnne bado ipo jikoni kidogo ila progress ni nzuri Mungu akijaalia atavaa jezi ya Yanga hivi karibuni”, alimaliza.
Usajili wa Mbuyu Twite, Yanga wanena haya.
Reviewed by Steve
on
Friday, July 10, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Friday, July 10, 2015
Rating:
