Simba wakiendelea na maandalizi, soma Kiiza anavyojitambia
Mshambuliaji wa Simba, Hamisi Kiiza ametamba kuwa kikosi anachokichezea kitafanya vema kuliko
wengi wanavyofikiria.
Kiiza amesema Simba imekuwa ikifanya maandalizi mazuri wakiwa wamejichimbia Lushoto.
“Wanaweza kuona kama hatujiandai, lakini tunafanya kila linalowezekana kuwa fiti kwa kufuata maelekezo ya walimu.
“Baadaye tutakuwa vizuri tu, acha kwanza tumalizie maandalizi,” alisema Kiiza.
Kiiza amerejea nchini baada ya kuwa ameachwa na Yanga na kutimka nchini.
Lakini Simba imemnasa na kumsajili kwa miaka miwili huku Simba wakiwa wana imani kubwa kuwa atakuwa tishio katika umaliziaji.
Simba wakiendelea na maandalizi, soma Kiiza anavyojitambia
Reviewed by Steve
on
Thursday, July 16, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Thursday, July 16, 2015
Rating:
