Propellerads

Xavi afunguka nani atakua mkali wa dunia baada ya Messi.




Aliekua kiungo mkongwe wa Barca, Xavi Hernandez amefunguka kua ni nani ataekalia
kiti cha Messi ikitokea Messi anastaafu.

Mkali huyo anaamini mbrazil Neymar ndiye atakaekua mchezaji bora wa dunia kwa miaka ijayo.

"Ana kipaji, Leo Messi akistaafu atakua naamini atakua mchezaji bora bila shaka" aliiambia UEFA.com.

"Anafanya makubwa akiwa na umri wa miaka 21,22 pekee, na kufanya hivyo ukiwa Barcelona si mchezo.

"Neymar anaenda kua na wakati mzuri, hafanyi makosa.

Xavi pia alisema kua Neymar ni mtu poa sana japo huripotiwa vibaya na baadhi ya wapinzani wake.

Neymar amefunga magoli 38 na kutoa usaidizi mara 11 katika michezo 50 na wakali hao wa Catalan.
Xavi afunguka nani atakua mkali wa dunia baada ya Messi. Xavi afunguka nani atakua mkali wa dunia baada ya Messi. Reviewed by Steve on Sunday, June 07, 2015 Rating: 5
Propellerads
Powered by Blogger.