Matola awapa somo Simba kuhusu Messi.
Mshambuliaji wa zamani wa Simba, Malota Soma, amewataka viongozi wa Simba kumaliza tofauti zao za kimkataba na
winga Ramadhani Singano ‘Messi’ vinginevyo winga huyo akiondoka Simba haitapata mchezaji wa aina hiyo kwa miaka 10 ijayo.
Matola ambaye alitamba Simba miaka ya 1980 hadi mwanzoni mwa miaka ya 90, alisema: “Ni ngumu kupata mchezaji hapa Tanzania mwenye kipaji cha kipekee kama alichokuwa nacho Messi kwa sasa.
“Wachezaji wengi hawatofautiani, wengi wana staili moja ya uchezaji, lakini Messi yupo tofauti kwani ana uwezo wa kipekee wa kufunga mabao, anapiga chenga kali, anatengeneza nafasi za mabao, anakaba bila ya kuogopa adui, lakini ni mchezaji mwenye nidhamu nzuri.
“Hivi mnafikiri kwa kizazi cha sasa mtapata wapi mchezaji wa aina hii?
“Nafikiri viongozi kama mmekosea, mwombeni radhi kisha mmalizane naye kwa manufaa ya Simba, bila hivyo shauri yenu.
“Nakumbuka mara ya mwisho kuona mchezaji wa aina yake ni mwaka 1993 kwa Abdul Mashine aliyekuwa Simba na Thomas Kipese Thomas walikuwa vizuri na hodari.”
Matola awapa somo Simba kuhusu Messi.
Reviewed by Steve
on
Sunday, June 07, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Sunday, June 07, 2015
Rating:

