Propellerads

Van Gaal: Depay ana nafasi kubwa ya kung'aa Man United.




Meneja wa mashetani wekundu, Luis Van Gaal ana imani kua Mephis Depay ana nafasi kubwa ya kua
mchezaji mkubwa Manchester United.

Depay aliyetokea PSV tayari ameshasaini mkataba wa miaka minne na mashetani hao wekundu ijumaa (jana).

"Namjua Mephis vizuri tangu tupo wote timu ya taifa ya uholanzi" Van Gaal aliiambia tovuti rasmi ya Manchester United.

"Ni mchezaji hodari chipukizi anayeweza kucheza nafasi yoyote"

"Itamchukua muda kuuazoea upepo wa Premier League, lakini sina shaka kua ana nafasi kubwa ya kua mchezaji mkubwa katika hii klabu, na pia amekuja sehemu sahihi kuendeleza kipaji chake"

Depay nae aliongeza kua alikua na furaha kufanya kazi na Van Gaal na anadhani ndie kocha bora zaidi ulimwenguni.

"Hii ndoto imekua ya kweli kwangu; kuchezea klabu kubwa duniani, na pia kufanya kazi na mtu ambaye naamini ni kocha bora ulimwenguni Louis van Gaal"

"Nina imani kubwa katika uwezo wangu, na najituma ili nifikie ndoto zangu. Nilikuepo PSV tngu nina miaka 12, na ninapenda kuwashukuru kwa kila kitu."
Van Gaal: Depay ana nafasi kubwa ya kung'aa Man United. Van Gaal: Depay ana nafasi kubwa ya kung'aa Man United. Reviewed by Steve on Saturday, June 13, 2015 Rating: 5
Propellerads
Powered by Blogger.