Van Gaal afunguka kua umaarufu wa Man United ulimshangaza!!
Meneja wa Manchester United, Louis van Gaal amefunguka kua umaarufu ilionao klabu yake ya Manchester United
ulimshangaza katika ziara ya kabla ya msimu ya timu, msimu uliopita.
Man United walicheza mbele ya mashabiki 109,318 huko Michigan majira yaliyopita ya kiangazi, mabapo waliwachapa Real madrid 3-1 katika mechi ya kirafiki.
Akitathmini ziara ya mwaka jana, Van gaal aliiambia Daily Mail "ni ktu ambacho ilikua ngumu kuamini. Zilikua ni siku za mwanzo za umeneja wangu, jinsi mashabiki walivyokua na shauku pia na idadi yao ilikua ngumu kuamini"
"Tulicheza michezo kama minne au matano, na kulikua na mashabiki 300 000 katika wiki mbili pekee."
Mholanzi huyo aliongeza "Nikiwa naelekea kituo cha mafunzo cha AON, nafikiria kutakua na watu zaidi ya 100 wanaotaka nisaini fulana au picha zao na wengi wanatoka Asia"
"Huwezi kuamini jinsi Manchester United ilivyo maarufu"
Mwezi wa April Manchester United walitangaza kua wataumana na Barcelona na Paris Saint Germain katik ziara ya michezo minne Marekani mwezi wa Julai.
Van Gaal afunguka kua umaarufu wa Man United ulimshangaza!!
Reviewed by Steve
on
Sunday, June 21, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Sunday, June 21, 2015
Rating:
