Mkwasa na Morocco kuchukua mikoba ya Nooj Stars.
Baada ya kutimuliwa kwa Kocha Mart Nooij, nafasi yao wanapewa wazawa wawili, Charles Boniface Mkwasa ambaye ni kocha msaidizi wa Yanga na Ahmed Morocco aliyewahi kuinoa Coastal Union na JKT Oljoro.
Taarifa za ndani kutoka TFF, zinaeleza Mkwasa ndiye amekuwa chaguo la kwanza baada ya kikao cha dharura cha kamati ya utendaji.
“Mkwasa ndiye amepewa nafasi, msaidizi wake atakuwa ni Morocco. Wao ndiyo watapewa jukumu la kuisaidia Taifa Stars katika mechi dhidi ya Uganda kule kampala.
“Baada ya hapo, TFF itaendelea na mchakato wa kusaka kocha mpya wa kigeni,” kilieleza chanzo.
Mkwasa na Morocco kuchukua mikoba ya Nooj Stars.
Reviewed by Steve
on
Sunday, June 21, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Sunday, June 21, 2015
Rating:
