"Barca inaweza kuchukua ubingwa mara nyingi kila msimu"
Kiungo wa FC Barcelona, Sergio Busquets, anaamini wanaweza kuchukua ubingwa mara nyingi (treble) kila
msimu.
Wakali hao wa Catalan, wamechukua makombe matatu (treble) kwa mara ya pili msimu uliopita, huku wakiwahi tena kuchukua mara tatu enzi za Pep Guardiola akiinoa klabu hiyo.
Busquets anaamini kua wana timu yenye chipukizi na vijana wengi ambao wana uwezo na nia ya kufanya makubwa na kuchukua makombe mengi.
"Furaha ya ushindi hapa ni ya kudumu, haiwezi kuondoka" aliiambia El Pais
"Kila unachohitaji ni zaidi, zaidi na zaidi, tuna wachezaji wenye ubora mkubwa sana, timu yenye vipaji chipukizi wengi, na nafasi ya pekee kuonesha uwezo "
"Kwenye fainali ya mabingwa Ulaya, kama ukimtoa Dani Alves, Javier Mascherano na Andres Iniesta, sidhani kama kutakua na mchezaji zaidi ya miaka 30 kwenye timu yetu.
"Marc-Andre Ter Stegen ni kipaji chipukizi na Neymar, na Jordi Alba, tuliobaki tupo kati ya miaka 23-28
"Tunaweza kushinda Treble kila mwaka, tuna uwezo mkubwa"
"Barca inaweza kuchukua ubingwa mara nyingi kila msimu"
Reviewed by Steve
on
Sunday, June 21, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Sunday, June 21, 2015
Rating:
