Propellerads

Scholes "Ulimwenguni hakuna beki wa kumdhibiti Messi"




Mkongwe wa Manchester United, Paul Scholes anaamini kua hakuna beki yeyote ulimwenguni kwa sasa anaeweza
kumdhibiti nyota wa FC Barcelona,Lionel Messi kikamilifu.

Japokua Messi hakuweza kufunga kwenye fainali ya UEFA jana (jumamosi) usiku, lakini alitoa mchango kwenye goli alilofunga Luis Suarez.

Hadi michuano ya UEFA inamalizika, Messi amemaliza akiwa ni miongoni mwa vinara wa ufungaji akiwa na magoli 10, akiwa sambamba na wakali wengine kama vile Cristiano Ronaldo na Neymar ambao nao wana magoli 10 kila mmoja.

Kucheza na Messi, kama nilivyosema mwanzo ni zoezi gumu sana linalohitaji umakini wa hali ya juu" Scholes kama alivyonukuliwa na London Evening Standard.

"Wakati wowote mchezoni anaweza kukuchomoka, nguvu inahitajika, lakini hata akili pia, huwezi kupumzika hata kidogo"

"Sekunde ambayo utazubaa.....hayupo!!, ameondoka na mpira kuelekea golini, yaani kwa wewe kuzubaa sekunde tu."

Hakuna beki inayoweza kumdhibiti Messi kwa sasa. Lakini safu imaraya ulinzi inaweza kufanya hivyo.
Scholes "Ulimwenguni hakuna beki wa kumdhibiti Messi" Scholes "Ulimwenguni hakuna beki wa kumdhibiti Messi" Reviewed by Steve on Sunday, June 07, 2015 Rating: 5
Propellerads
Powered by Blogger.