Mavugo wa Simba avutiwa na nyota huyu wa Ulaya.
Mshambuliaji mpya wa Simba, Laudit Mavugo anaonekana kuvutiwa zaidi na Didier Drogba.
Mavugo anavutiwa na Drogba raia wa ivory Coast na amekuwa shujaa wake.
Straika huyo ameuambia mtandao mmoja maarufu kwamba anavutiwa na uchezaji wa Drogba katika ushambuliaji.
"Unajua Drogba ni mchezaji wa aina yake, mshambuliaji anayejua kazi yake kabisa. Ananivutia sana pia napenda kumuona anacheza," alisema.

Drogba ambaye amerejea Chelsea na kuiwezesha kubeba tena ubingwa wa England, pia amekuwa chaguo namba moja la mshambuliaji wa zamani wa Simba, Selemani Ndikumana.
Ndikumana, raia wa Burundi kama ilivyo kwa Mavugo, amewahi kuichezea Simba kwa misimu miwili kabla ya kuondoka na kwenda Ubelgiji, Rwanda na baadaye Sudan.
Mavugo wa Simba avutiwa na nyota huyu wa Ulaya.
Reviewed by Steve
on
Sunday, June 07, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Sunday, June 07, 2015
Rating: