Propellerads

Pamoja ya kuwemo wakali Busungu, Kaseke, Kessy, Stars yachapwa.




Kikosi cha Taifa Stars kinachoundwa na vijana wengi, kimelala kwa mabao 2-0 dhidi ya wenyeji wake Rwanda.

Katika mechi hiyo iliyochezwa kwenye Uwanja wa Amavubi jijini Kigali, wenyeji walipata bao kila kipindi.

Bao la kwanza la Rwanda lilifungwa na Patrick Sibomana kabla ya Yannick Mukunzi kufunga la pili katika kipindi cha pili.

Rwanda ndiyo walionekana kutawala zaidi nafasi ya kiungo na kuipa wakati mgumu Stars.

Pamoja na juhudi za Kocha Salum Mayanga kuwatoa Hassan Dilunga na Kelvin Friday na nafasi zao kuchukuliwa na Deus Kaseke na Atupele Green, bado mambo hayakuwa mazuri.

Mayanga hakuchoka, alimtoa Mudathir Yahya na nafasi yake kuchukuliwa na Malimi Busungu, lakini bado hakukuwa na mabadiliko matokeo.

KIKOSI CHA STARS KILICHOANZA:
SAID MOHAMMED
RAMADHANI KESSY
MOHAMMED HUSSEIN ‘TSHABALALA’
ISIHAKA HASSAN
SIMWANZA EMMANUEL
MUDATHIR YAHYA
HASSAN DILUNGA
AMRI KIEMBA
KELVIN FRIDAY

RASHID MANDAWA
Pamoja ya kuwemo wakali Busungu, Kaseke, Kessy, Stars yachapwa. Pamoja ya kuwemo wakali Busungu, Kaseke, Kessy, Stars yachapwa. Reviewed by Steve on Sunday, June 07, 2015 Rating: 5
Propellerads
Powered by Blogger.