Mkwasa afunguka kuhusu kuifundisha Stars.
Kocha msaidizi wa klabu ya Yanga Charles Boniface Mkwasa ‘Master’ amekuwa akitajwa kurithi mikoba y
a aliyekuwa kocha mkuu wa kikosi cha timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ Mart Nooij kufuatia kocha huyo kutimuliwa baada ya Stars kubanwa na kutandikwa goli 3-0 na timu ya taifa ya Uganda kwenye mchezo wa kuwania kufuu kucheza fainali za mMataifa ya Afrika kwa wachezaji wanao cheza ligi za ndani (CHAN) uliopigwa Zanzibar jana usiku.
Mkwasa amesema bado hajapokea taarifa rasmi kutoka TFF ila yupo tayari kukifundisha kikosi cha timu ya Taifa endapo atatakiwa kufanya hivyo. Amefafanua kuwa, yeye kwasasa bado ni mwajiriwa wa Yanga kwahiyo ni lazima taratibu zifuatwe ili aweze kukichukua kikosi cha Stars.
“Kusema kweli nimezisikia taarifa za kutaka kupewa mikoba ya kukinoa kikosi cha Stars lakini nasubiri mpaka tutakapokuwa tumeongea kwasababu mimi bado ni mwajiriwa wa Yanga kwahiyo baada ya kupata taarifa tutafanya taratibu zinazotakiwa. Kwasababu mimi nimekuwa nasikia tu kutoka kwenye vyombo vya habari lakini watakapokuwa wameniambia ‘officially’ basi tutajaribu kuangalia hali halisi ya timu tutaiwekaje”, Mkwasa amesema.
“Kutokana na mchezo wa jana siwezi kusema moja kwa moja kitu kipi kimetuua lakini ukiangalia kwa harakaharaka utagundua kulikuiwa na matatizo ya kiufundi kidogo, kwa maana kwamba kulikuwa na hitilafu katika ulinzi kwasababu kulikuwa na mabeki wanakwenda mbele kwa wakati mmoja na mambo madogomadogo mengine niliona pengine wachezaji wenyewe walikuwa hawajachangamka”, aliongeza.
“Sasa hizo ni sababu mbili-tatu ambazo niliziona lakini sikwenda kule kwasababu ya kufanya tathmini hiyo mimi nilikwenda kama mtanzania mwingine kwasababu kunawachezaji wangu pale kwenye ligi nilitaka kujua wapo kwenye kiwango gani kwasababu tumeanza mazoezi kwenye timu yetu”, alifafanua.
“Ni mapema sana kusema kitu chochote, ninachoweza kusema ni kwamba tusubiri hali itakapokuwa imekaa vizuri basi tutatoa taarifa kamili. Hili suala ni la kitaifa, ni kama yanavyotokea mafuriko, kwahiyo huwezi kusema unaziba daraja sasahivi, lazima utafute namna ya kutatua tatizo. Sasa maadam limeshazungumzwa, tusubiri litakapokuwa limekaa vizuri tutaliweka sawa”, alieleza.
Stars jana ilibanjuliwa goli 3-0 kwenye uwanja wa Amaan visiwani Zanzibar na kujiweka kwenye mazingira magumu ya kusonga mbele kwa hatua inayofuata kwani ili iweze kusonga mbele inahitaji ushindi wa kuanzia goli 4-0 ikiwa ugenini kwenye uwanja wa Namboole jijini Kampala, Uganda wiki mbili zijazo.
Mkwasa afunguka kuhusu kuifundisha Stars.
Reviewed by Steve
on
Monday, June 22, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Monday, June 22, 2015
Rating:
