Julio ajifagilia kuinoa Stars.
Kocha wa Mwadui FC, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ amesema akipewa nafasi ya kuinoa Taifa Stars, Watanzania
wataona kazi.
wataona kazi.
Julio amesema ana imani kubwa kama atapewa nafasi hiyo akiwa na Charles Boniface Mkwasa na Ahmed Morocco.
“Hakika ninaamini tulijitakia wenyewe. Kama wananiamini wanipe mimi pamoja na Mkwasa na Morocco.
“Najua kabisa Tanzania ina wachezaji wengi wenye uwezo wa kucheza na kuisaidia nchi. Achana na hisia kwamba Tanzania haina wachezaji,” alisema Julio.
TFF imemtimua aliyekuwa kocha wa Stars, Mart Nooij mara baada ya kikosi cha Stars kulala kwa mabao 3-0 dhidi ya Uganda, The Cranes.
Hata hivyo tayari Nooij alikuwa amepoteza kabisa uwezo wa kuisaidia kwa kipindi kirefu ingawa TFF ilionekana kutojiamini kuchukua maamuzi haraka.
Julio ajifagilia kuinoa Stars.
Reviewed by Steve
on
Monday, June 22, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Monday, June 22, 2015
Rating:
