Propellerads

Messi - mechi 100 bila taji lolote Argentina.




Nyota wa FC Barcelona na timu ya taifa ya Argentina, Lionel Messi, Jumamosi hii atacheza mchezo wa
100 kwa timu yake ya taifa huku bado akiwa hajachukua taji lolote kubwa akiwa na timu yake ya taifa.

Messi alianza kuichezea timu yake ya taifa tangu mwaka 2005, ambapo mchezo wa Jumamosi dhidi ya Jamaica michuano ya Copa America, utakua ni mchezo wake wa 100.

Akiongelea furaha yake kufikisha mchezo wa 100, alisema lengo lake kubwa ni kuchukua ubingwa.

"Nina furaha kubwa kufikia rekodi hii" aliongea kwa mujibu wa Daily Nation.

"Natumaini nitasherehekea ubingwa mwingine kwa mara ya kwanza, na pia kote kote nitakua nimenyanyua vikombe"

Alianza kuonekana katika timu ya taifa akiwa na miaka 18, lakini mechi yake ya kwanza iliisha kwa uchungu kwani alitolewa nje baada ya kumpiga kikumbo mchezaji katika timu pinzani.

Uchezaji wake katika timu ya taifa umekua ukikosolewa na wengi, wakidai sio kama anavyocheza akiwa na klabu yake ya Barcelona, lakini hata hivyo ana rekodi nzuri ya magoli 49 katika michezo 99.

Messi akiwa na timu ya taifa, tayari amefanikiwa kucheza fainali kubwa mbili, ya kwanza ni katika kombe la dunia 2914 ambapo walipoteza mbele ya Ujerumani, na nyingine ni fainali ya Copa America 2007 ambapo walipoteza mbele ya Brazil.
Messi - mechi 100 bila taji lolote Argentina. Messi - mechi 100 bila taji lolote Argentina. Reviewed by Steve on Friday, June 19, 2015 Rating: 5
Propellerads
Powered by Blogger.