Bahanuzi na tuhuma za kuidai Yanga.
Mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Said Bahanuzi amesema anataka Yanga imlipe kitita cha Sh milioni 17.
Bahanuzi amesema anahitaji kulipwa fedha hizo baada ya Yanga kukatisha mkataba wake.
“Tayari suala hilo linashughulikiwa na mwanasheria. Wanajua kuwa wanatakiwa kunilipa, hivyo naendelea kusubiri kutoka kwao,” alisema.
Hata hivyo Yanga ilishafafanua suala hilo na kusema Bahanuzi alicheza chini ya kiwango kitu ambacho kimkataba wanakuwa na uamuzi wa kuendelea naye au la.
Bahanuzi aliwahi kuisaidia Yanga kubeba Kombe la Kagame mwaka 2012 Yanga ikiwa chini ya Kocha Tom Saintfiet ambaye sasa ni kocha wa Togo.
Bahanuzi na tuhuma za kuidai Yanga.
Reviewed by Steve
on
Friday, June 19, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Friday, June 19, 2015
Rating:
