Propellerads

Wachezaji Stars wamkandia mzungu wao

Hali inaonekana kuwa si shwari katika kikosi cha timu ya taifa, Taifa Stars, ambapo inadaiwa kuwa kuna mgawanyiko ndani ya kikosi hicho ambacho kipo katika michuano ya Cocafa nchini Afrika Kusini.
            
Stars

Baadhi ya wachezaji wa Stars wamezungumza na mtandao mmoja na kusema hawafurahishwi na jinsi timu hiyo inavyocheza na kudai kuwa kila wanapomshauri kocha wao, Martin Nooij amekuwa haelewi somo, ndiyo maana wanafanya anavyotaka yeye.

“Tumemwambia mara nyingi kuwa sisi wachezaji tunajuana wenyewe lakini amekuwa mbishi,” alisema mchezaji mmoja.

Upande wa Nooij akizungumzia matokeo mabaya ya Stars katika Cosafa, alisema mashindano hayo hayakuwa na umuhimu kwake na badala yake anatumia kama maandalizi ya kucheza na Misri.

Wakati huohuo, Stars inatarajiwa kurejea nchini leo usiku mara baada ya mchezo wa kukamilisha ratiba dhidi ya Lesotho utakochezwa leo jioni.

Aidha, Kamati ya Utendaji ya TFF inatarajiwa kukutana keshokutwa Jumapili ambapo moja ya ajenda itakua ni kupokea na kujadili mienendo, maandalizi na maendeleo ya timu za taifa.

Wachezaji Stars wamkandia mzungu wao Wachezaji Stars wamkandia mzungu wao Reviewed by Steve on Friday, May 22, 2015 Rating: 5
Propellerads
Powered by Blogger.