Propellerads

Stand nao waonesha jeuri ya pesa.....waingia kwa huyu

Uongozi wa Stand United ya Shinyanga umefunguka kuwa unamnyemelea beki wa kati wa Mtibwa Sugar, Salim Mbonde ambaye anadaiwa kufuatiliwa na timu za Simba na Yanga.

Mbonde
                                         

Stand ambayo imepanga kujiimarisha zaidi katika ligi msimu ujao baada ya kunusurika kushuka daraja, imeeleza kuwa inahitaji kufanya usajili makini ili kuweza kuleta ushindani msimu ujao.

Muhibu Kanu ambaye ni Mkurugenzi wa Benchi la Ufundi la Stand, amesema moja ya mikakati waliyojiwekea katika timu hiyo ni kuhakikisha wanakuwa na kikosi kilicho bora zaidi, ndiyo maana wanaendelea kusaka wachezaji wenye viwango vya juu.

“Tupo katika mazungumzo na Salum Mbonde ili tumsajili, tunajua kwa sasa yupo katika timu ya taifa lakini atakaporejea nchini ndiyo tutajua hatma yake.

“Tuna mikakati mikubwa kwa ajili ya msimu ujao, kwani tunahitaji kuwa na kikosi bora kwa kusaka kipa imara ambapo kwa sasa tunafanya mazungumzo na Juma Kaseja ili aweze kuziba pengo la kipa kutokana na mtazamo wetu kuwa atatufaa, kwani malengo yetu ni kumaliza katika ‘top four’ msimu ujao.

“Kaseja mwenyewe ameonyesha nia ya kuja kuichezea timu yetu ambapo ametutaka tufanye mazungumzo na meneja wake,” alisema Kanu.
Stand nao waonesha jeuri ya pesa.....waingia kwa huyu Stand nao waonesha jeuri ya pesa.....waingia kwa huyu Reviewed by Steve on Friday, May 22, 2015 Rating: 5
Propellerads
Powered by Blogger.