Unawajua mabeki ngangari wa Suarez!!.....mwenyewe awataja.
Mchezaji huyo wa zamani wa Liverpool amewataja walinzi ambao anadai walimpa wakati mgumu sana na pia hakufurahi kila alipopambana nao kipindi akichezea ligi kuu ya Uingereza.
Alisema EPL ina mabeki wengi wakali, warefu, imara lakini wapo sita ambao kwake walikua ni mwiba.
"England wapo mabeki wengi , wana nguvu, ni warefu na pia ni imara. Mwangalie John Terry, Gary Cahill, Phil Jones, Vincent Kompany, Branislav Ivanovic, Laurent Koscielny-wapo wengi wenye nguvu, mabeki imara Premier League" aliiambia Squawka.
"Nilikua na mpambano nao, lakini pia ni namna unavyocheza nao. Kama ukinipa mpira mrefu mbele ya hao mabeki, sitaweza kuwashinda.
"Lakini jinsi Liverpool ilivyocheza, mpira uwanjani, kisha ukapigwa haraka kwangu, ilinipa nafasi zaidi. Tulijituma sana kupata njia abazo tungewahadaa mabeki, mtu kwa mtu.
"
hio ndio njia pekee nilikua nafanikiwa England, ikimaanisha mabeki imara ni wale waliokua na kasi pia, ambao waliniweka katika mpambano kwa staili hiyo"
Suarez kwa sasa anajiandaa na klabu yake ya Barcelona kwa ajili ya fainali ya Uefa dhidi ya Juventus June 6.
Unawajua mabeki ngangari wa Suarez!!.....mwenyewe awataja.
Reviewed by Steve
on
Friday, May 29, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Friday, May 29, 2015
Rating:
