Nyota watano ambao wanaweza kuondoka Manchester United.
Robin van Persie
Mholanzi huyu amekua nje ya kiwango chake msimu huu, hali inayotizamiwa na wengi Van Persie mwenye miaka 31 anaweza asiwemo kwenye kikosi kijacho cha kocha Louis van Gaal. Majeraha yalimuandama sana msimu huu na inaaminika kua Man U bado wanasita kumuongeza mkataba mwingine. Bado haijaeleweka ni wapi haswa ataelekea endapo ataondoka klabuni hapo, ingawa baadhi vikubwa Serie A vinaonesha kuvutiwa nae.
Angel Di Maria.
Baada ya kuhangaika msimu huu ili kudhihirisha uthamani wa dau lake la usajili, inaaminika Di Maria anaweza kuondoka dirisha la usajili litakapofunguliwa.Zimekuwepo ripoti za yeye kuwindwa na vilabu kama Paris Saint Germain na Bayern Munich, lakini bado haijathibitika kama ni kweli ataondoka au ataendelea.
David De Gea
Mlinda mlango huyu nyota amekua ni miongoni mwa wachezaji muhimu zaidi wa Man U msimu huu, lakini Real Madrid wameonesha nia ya kutaka kuipata saini ya mkali huyu. Mhispania huyo anatarajiwa kumrithi Iker Casillas Santiago Bernabeu.
Rafael
Mbrazil huyo hajaonekana sana msimu huu kutokana na kukabiliwa na majeraha, lakini haijaeleweka bado kama ataweza kurejea kikosini pindi atakapokua sawa. Inaonekana Man U wanaweza kumruhusu ashike njia kipindi cha usajili, kwani Antonio Valencia anaonekana kuimudu nafasi yake vizuri pia.
Adnan Januzaj
Mwanzoni mwa msimu huu, kocha Van Gaal alionesha imani kubwa na mchezaji huyu, lakini hata ivyo hivi karibuni imekua ni ngumu sana kwake kupata nafasi kubwa katika kikosi. Januzaj bado ana kipaji na inasemekana anaweza kuondoka kwa mkopo wa muda mrefu kuelekea klabu yake ya zamani PSV Eindhoven ambao nao wanadaiwa kutafuta winga.
Nyota watano ambao wanaweza kuondoka Manchester United.
Reviewed by Steve
on
Friday, May 29, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Friday, May 29, 2015
Rating:
