Propellerads

Chelsea nao wanamnyemelea Ronaldo.


                           
              

Klabu ya Chelsea nao pia wako katika kinyang'anyiro cha kuiwinda saini ya nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo, vyombo vya habari nchini Uingereza vimeripoti.


Inaaminika kua mreno huyo anaweza kufunguliwa milango ya kuodoka klabuni Los Blancos, ambapo inadaiwa wana mpango wa kumpa nafasi zaidi Bale apate kung'aa pia.

Hatma ya Ronaldo klabuni imekua ni ya mashaka zaidi hasa wakati huu, pia ujio wa kocha mpya unaweza kua sababu kubwa itakayomtoa Ronaldo.

Kulingana na gazeti la Daily Star Chelsea wako katika mipango ya kumnasa mkali huyo kwani wameonesha nia ya kuuhutaji mchango wake darajani.

Ada ya uhamisho wa Ronaldo inadaiwa itakua inaanzia pauni mi. 71.5, ambapo pia Man U nao wametajwa kua katika harakati za kutaka kumrudisha nyota wao huyo wa zamani.

Kwa ujio wa Benitez kama bosi mpya, inadaiwa tena klabu itapendelea zaidi kumtumia Bale msimu ujao na kumng'arisha kama nyota wao na wako tayari kumwachia Ronaldo aondoke.

Miezi ya hivi karibuni kumekuepo na tetesi kua kati ya Bale au Ronaldo kuna uwezekano mkubwa wa mmoja kati yao kuondoka klabuni hapo.

Chelsea nao wanamnyemelea Ronaldo. Chelsea nao wanamnyemelea Ronaldo. Reviewed by Steve on Friday, May 29, 2015 Rating: 5
Propellerads
Powered by Blogger.