Tetesi: Mourinho anamtaka Zlatani
![]() |
| Zlatan akiwa na Mourinho |
Kuna tetesi zinasema kua bosi wa Chelsea "The super one" anaiwinda
saini ya fowadi wa PSG Zlatan Ibrahimovic.
Akiwa amebakiza mwaka mmoja katika mkataba wake na klabu yake ya sasa, ripoti zinadai hatua inayofuata kwake ni kujiunga na kocha huyo mreno pale darajani.
Msweden huyo alicheza chini ya Mourinho pale Inter Milan na kufanikiwa kuchukua taji la Serie A 2008/09, ambapo Metro wameripoti kua bosi Mourinho anataka kufanya suprise hiyo mwishoni mwa msimu huu.
Hata ivyo imeripotiwa Mourinho na Ibrahimovic hua wana uhusiano wa karibu ambapo ilidhihirika pia pale Mourinho alipomtetea Zlatan baada ya kadi nyekundu katika michuano ya UEFA kati ya Chelsea na PSG.
Pia Zlatan alihusishwa na kutaka kujiunga Liverpool, lakini yaonekana mchezaji huyo anataka kuingia vilabu vilivyopo ligi ya mabingwa ulaya.
Zlatani amepata kuchezea vilabu vikubwa ulaya kama vile Juventus, Barcelona, Ajax Amsterdam, lakini hajawahi kucheza klabu yoyote ya Uingereza.
Msimu huu Zlatan amecheza mechi 36 akifunga magoli 30,huku akitoa usaidizi zaidi ya mara nane.
Tetesi: Mourinho anamtaka Zlatani
Reviewed by Steve
on
Thursday, May 21, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Thursday, May 21, 2015
Rating:
